Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:47

Uchunguzi wa mauaji ya mbunge wa Uingereza unaendelea


Picha ya mbunge Jo Cox aliyepigwa risasi Uingereza
Picha ya mbunge Jo Cox aliyepigwa risasi Uingereza

Wachunguzi wa polisi katika halmashauri ya Yorkshire kaskazini mwa Uingereza ambayo ilikuwa inawakilishwa na mbunge Jo Cox aliyeuwawa, wanakataa kuthibitisha au kukanusha kwamba mshukiwa aliyefanya mauaji hayo amechochewa na imani za utaifa za mrengo wa kulia.

Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 41 na ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa alipigwa risasi na kuchomwa kisu mbele ya watu na Thomas Mair, mwenye umri wa miaka 52 huku akisema “Uingereza kwanza.”

Chama kidogo cha kisiasa cha mrengo wa kulia 'Britain First' ambacho kinafanya kampeni kwa miaka mingi kwa nchi hiyo kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya, kilisema hakikuhusika katika mauaji ya mbunge huyo anayeunga mkono umoja wa ulaya na uongozi wake ulilalamikiwa kwa shambulizi.

XS
SM
MD
LG