Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 06, 2025 Local time: 15:36

Juhudi za kutokomeza uhasama wa kisiasa kabla ya uchaguzi Kenya


Majaji wa Mahakama ya Rufaa wakitoa uamuzi
baada ya NASA kuipeleka Jubilee Mahakamani kutafuta ufumbuzi wa kisheria.
Majaji wa Mahakama ya Rufaa wakitoa uamuzi baada ya NASA kuipeleka Jubilee Mahakamani kutafuta ufumbuzi wa kisheria.

Kwa takriban miaka kumi sasa Kenya imekuwa ikikumbwa na wasiwasi wa kushuhudia machafuko wakati uchaguzi mkuu unapokaribia.

Sababu moja ni uhasama wa kisiasa unaotokana na kasumba ya ukabila, na hivyo kusababisha chuki baina ya wanasiasa au hata jamii moja kwa nyingine.

Uchaguzi mkuu wa Kenya unatarajiwa kufanyika Agosti 8. Makala hii inaangazia hali ya usalama na zoezi la upigaji kura kupata viongozi wapya.

Kamishna mkuu anayesimamia utawala eneo la Pwani ya Kenya, Nelson Marwa anaelezea jinsi suala la usalama lilivyo juu katika maeneo yote ya nchi hiyo na kuwasihi wagombea kuheshimu kanuni na taratibu wa uchaguzi ili kudumisha amani wakati wa kampeni.

“Kama unataka kuwa mbunge utafute kiti kwa utaratibu tusianze kutumia vijana kubeba visu, hivi visu utabeba mpaka mwaka gani, “ amehoji Marwa.

Mchango wake wa kuimarisha usalama umeigwa na kuenziwa kote Kenya.

Kwa wenyeji wa Mombasa wanafahamu vyema kauli hizo zinavyoweza kuharibu yote yaliyo mazuri ambayo yanatiliwa mkazo na kila mkazi, kama anavyosema Omar Kombo mwenyeji wa Mombasa.

“Ule mtaa mimi naishi kuna vijana ambao wanaumiza watu kwa njia moja ama nyingine, na huoni mwanasiasa hata mmoja anayezungumza na wana habari azungumzie hasa suala la usalama kujadili kwamba sehemu fulani kuna genge la wahuni wanaumiza watu lakini wao wanao raha polisi akiuawawa, wakijihisi wanao wanadhulumiwa lakini wanasiasa ndiyo hasa huwatumia hawa vijana.”

Wakati huu wote ambao kampeni za kisiasa zimechacha, maafisa wa usalama kwa pamoja wamekuwa macho kuzuia visa vya uhalifu, japo wakuu wa usalama wakisisitiza kuwa usalama ni jukumu la kila mwananchi.

Raia wengi waliozungumza na Sauti ya Amerika wanasema wakati wa kusubiri polisi mitaani umekwisha, wao wanajipanga kuwakabili na hata kuwatimua wahuni.

Licha ya hamasa zote hizi makundi yanayochipuka ni mengi kila mahali nchini humo, na zaidi sehemu zenye mizozo. Mara kwa mara serikali imekuwa ikipiga marufuku makundi haramu yanayojumuisha magenge ya wahalifu.

Ukosefu wa usalama umehusishwa pakubwa na siasa za chuki nchini Kenya. Chuki hii kwa kiasi kikubwa inahusishwa na ukabila.

Bi Mercy Otieno ni mfanya-biashara, lakini anapojiandaa kupiga kura Agosti 8 ana mengi ya kuwaasa wapiga kura wenzake kutenda yaliyo mema ili uchaguzi ufanyikekwa amani na utulivu.

“Kuna tatizo la kupiga kura hapa kwetu, ukabila umezidi sana. Nikitoka nikienda town kununua vitu zangu za biashara nasikia mtu anasema huko dukani, uzia watu wa NASA haraka watoke nje. Nimeshindwa watu wa NASA ni watu gani na watu wa Jubillee ni watu gani huko Kenya watu wamoja,” anahoji Otieno.

Elimu ya kijamii imekuwa pia ikitolewa kwa wananchi, kuelewa umuhimu wa kupiga kura kutokana na uadilifu wa watu, badala ya kuhongwa.

Uchaguzi mkuu wa Kenya mapema mwaka 2013 haukuwa na ghasia ikilinganishwa na uchaguzi mwingine wa mwaka 2007, lakini visa kadhaa viliripotiwa.

Bwana Marwa anasema polisi imeweka mikakati thabiti kukabiliana na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani, “ukianza kuongea mambo ya insecurity unaambiwa unaigilia viongozi, yaani hapa Majengo tu, mtu anabadilisha nyumba inakuwa armory. Hakuna kubembelezana hapa kwa masual ya maisha ya wananchi, mambo ya kutumia vijana kuvurugana mitaani yaishe, wakenya wote ni binadamu.”

Mashirika kadhaa ikiwemo tume ya Ulaya yameripoti uwezekano wa kuzuka vurugu wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu.

Sauti ya Amerika upande wake ina ushahidi jinsi watu wanapanga kuhamiamaeneo yaliyo salama ili kujiepusha na uwezekano wa ghasia, japo hisia nyingi zinatolewa kwa usiri mkubwa.

Matukio hayo yaliadhiri wengi. Maelfu ya Wakenya bado wana makovu ya mwilini na wengine ya moyoni.

Lakini matumaini ya uchaguzi wa amani yangalipo.

Chini ya katiba mpya ya Kenya uchaguzi mkuu utafanyika kwa mara ya pili

Agosti 8, na waliojitokeza kugombea urais pia ni watu wanane.

XS
SM
MD
LG