Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 19:02

Jinsi Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (BAL) inavyokuza vipaji


Sherehe za ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu BAL Kigali
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:45 0:00

Sherehe za ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu BAL Kigali

Ligi maarufu zaidi duniani katika mpira wa kikapu NBA inayochezwa Marekani ina mchakato mpana wa kuwatambua na kuwashirikisha vijana walio na vipaji katika mchezo huo.

NBA inatekeleza mchakato huo kupitia taasisi mbali mbali za elimu na michezo katika babara yote duniani.

Katiba bara la Afrika ushirikishaji huo unafanikiwa kupitia chuo cha mpira wa kikapu NBA Academy Africa kilicho huko Saly Senagal,Magharibi mwa Afrika.

National Basketball Association (NBA) ilizindua chuo hicho mwaka 2017 kwa lengo la kuwapa elimu na mafunzo ya mpira wa kikapu, wachezaji chupikizi barani Afrika.

“Tunatazamia kuwa NBA Academy Africa inajenga na kuendeleza azma ya wachezaji chipukizi katika bara hili na kuwawekea mazingira ya kufaulu zaidi”, alisema afisa wa NBA Amadao Gallo Fall alipoongoza uzinduzi wa chuo hicho 2017.

Katika muda wa miaka mitano iliyopita wanafunzi waliokuzwa katika chuo hicho tayari wamecheza mpira wa kikapu na kufikia upeo wa juu mchezo wa kulipwa.

Mapema mwaka 2023 waandaaji wa Basketball Africa League (BAL) walitangaza kuwa wachezaji-wanafunzi 12 kutoka NBA Academy Africa wangejianga na timu 12 zilizoratibiwa kucheza ligi ya BAL 2023 chini ya Programu ya BAL Elevate – kila timu ikiruhusiwa kuwa na mchezaji mmoja katika mechi za vitengo vya Sahara Conference (Darkar) na Nile Conference (Cairo).

Vijana hao kutoka nchi 7 za kiafrika ni Joy Ighovodja (Nigeria), Khaman Maluach (Susan Kusini), Khadim Mboup (Senegal), Ulrich Chomche (Cameroon), Reuben Chinyelu (Nigeria), Churchill Abass (Nigeria), Dramane Camara (Mali), Parby Kabamba (DR Congo), Segun Obe (Nigeria), Paul Mbiya (DR Congo), Seifeldin Hendaway (Misri), na Mabilmawut Mabil (Sudan Kusini).

Timu mbili za Afrika Mashariki ziliwapata vijana wawili wchezaji kutoka NBA Academy Africa, ambapo Ulrich Kamka Chomche wa Cameroon alijiunga na Rwanda Energy Group (REG) ya Rwanda, naye Segun Ezekiel Obe wa Nigeria akaitwa kuchezea mabingwa wa Uganda City Oilers iliyo na makao katika mji wa Kampala.

“Tumepokea ripoti za kusisimua kutoka kwa makocha pamoja na timu zilizopokea wanafunzi wetu wa awali hapa NBA Academy Africa tangu tulipoanza mwaka 2017-2018. Wamechangia pakubwa kuinua kiwango cha mchezo huu, na baadhi walisajiliwa kucheza katika ligi ya NBA kiwango cha G”, aliongeza Amadao Gallo Fall akiwa katika makao makuu ya BAL huko Darkar, Senegal.

Timu 8 zilizofuzu kwa fainali ya ligi ya mpira wa kikapi Afrika (BAL 2023) kuanzia Mei 20 hadi Mei 27, kila moja iliwakilishwa na mchezaji mmoja mwanafunzi kutoka NBA Academy Africa.

Timu hizo ni Al Ahly ya Misri, Stade Malien ya Mali, Cape Town Tigers ya Afrika Kusini, AS Douanes ya Senegal, Ferroviario da Beira ya Msumbiji, Petro de Luanda ya Angola, Abidjan ABC Fighters ya Ivory Coast, na wenyeji Rwanda Energy Group (REG) ya Rwanda.

Wawakilishi wengine wa Afrika Mashariki City Oillers ya Uganda waliondolewa kwenye mechi za mwondoano kitengo cha Nile Conference huko Cairo Misri, waliposajili ushindi mmoja pekee na kupoteza mechi 4.

Wakati wa mechi za fainali huko Kigali Rwanda, wachezaji chipukizi kutoka NBA Academy Africa walijumuika ndani ya ukumbi wa BK Arena ili kufuatilia michezo yote kuanzia robo fainali hadi fainali.

Waandaaji wa mashindano ya BAL wanasema yapo matumaini makubwa kwa vijana hao kucheza katika ligi kuu ya NBA miaka inayokuja.

VOA imeshirikiana na NBA kuleta matangazo ya michuano ya 3 ya BAL 2023.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Josephat Kioko, Kenya

Forum

XS
SM
MD
LG