Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 22, 2023 Local time: 16:56

Jinsi kibali cha kuona siri za serikali kinavyotolewa Marekani


Rais Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump Jumatano alitengua kibali cha kuona siri za serikali cha Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA), John Brennan. Je, kitendo hicho kina maanisha nini?

Katika serikali ya Marekani kuna aina tatu za siri : Confidential, Secret na Top Secret. Vibali vya kuona ripoti za siri havimaliziki muda wake. Lakini, kibali cha Top Secret kina chunguzwa kila baada ya miaka mitano, kibali cha Secret kinachunguzwa kila baada ya miaka 10 na kibali cha Confidential kinachunguzwa kila baada ya miaka 15.

Nani wanapatiwa vibali vya kuona siri za serikali?

Kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya serikali inayosimamia majukumu iliyotolewa mwaka 2017, kiasi cha watu milioni 4.2 walipatiwa vibali vya kuona ripoti za siri hadi kufikia mwaka 2015, wakiwemo maafisa wa jeshi, wafanyakazi wa umma, wafanyakazi walioingia mikataba na serikali.

Kwa nini kibali cha kuona ripoti za siri kinahitajika unapokuwa umestaafu?

Maafisa wa ngazi ya juu wa usalama waliostaafu na maafisa wa jeshi wanahitaji vibali vya kuona ripoti za siri iwapo wataitwa kutoa ushauri katika masuala nyeti.

Je, rais anaweza kutengua kibali cha kuona ripoti za siri?

Anaweza kufanya hivyo. Lakini hakuna kumbukumbu ya kuwa rais amewahi kutengua kibali cha kuona ripoti za siri cha mtu yoyote. Kibali cha kuona ripoti za siri kawaida kinatenguliwa na idara ya serikali iliyomuombea kibali hicho mfanyakazi wake au mtu aliyeajiriwa kwa mkataba.

Idara zote za serikali kuu zinafuata orodha ya vigezo 13 vinavyo halalisha kutengua au kumnyima mtu kibali ambavyo vinaweza kuhusisha vitendo vya uhalifu wa jinai, kukosekana uaminifu kwa taifa la Marekani, tabia au hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa taifa au uvunjifu wa usalama.

XS
SM
MD
LG