Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 03:12

Jeshi na polisi Nigeria zatofautiana kuhusu ripoti ya usalama


Baadhi ya wasichana waliobaki ambao walitekwa kutoka mji wa Chibok
Baadhi ya wasichana waliobaki ambao walitekwa kutoka mji wa Chibok

Jeshi na polisi la Nigeria siku ya Jumatatu lilitofautiana hadharani juu ya mpangilio wa usalama katika mji wa kaskazini-mashariki mahala ambako wasichana 110 walitekwa nyara na washukiwa wanamgambo wa Boko Haram.

Kulingana na taarifa ya shirika la habari la Reuters jeshi lilitoa taarifa ambayo ilisema wanajeshi waliondolewa kutoka Dapchi katika jimbo la Yobe kabla wasichana kutekwa kutoka shule ya mji wao na waasi wenye silaha hapo Februari 19. Shambulizi hilo ni moja ya utekaji nyara mkubwa sana tangu utekaji wa Chibok mwaka 2014 ambapo zaidi ya wasichana wa shule 250 walichukuliwa na kundi la wanamgambo wa ki-Islam.

Tukio hili limechochea maswali kuhusu uwezo wa vikosi vya usalama nchini humo kupambana na waasi ambapo serikali mara kwa mara inaeleza kwamba imewashinda waasi. Wanajeshi waliopelekwa mwanzoni huko Dapchi walihamishwa na kupelekwa kuongeza nguvu za wanajeshi waliokuwepo Kanama kufuatia shambulio dhidi ya wanajeshi. Hali hiyo imezusha mvutano kati ya jeshi na polisi, lakini hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

XS
SM
MD
LG