Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 01:09

Jeshi la Burundi lakabiliwa na migogoro


Rais Pierre Nkurunziza

Miaka miwili imeshapita sasa, lakini kuna dalili ndogo sana ya mgogoro wa Burundi kupatiwa ufumbuzi.

Kwa mujibu wa ripoti iliotolewa na Kikundi cha kimataifa cha International Crisis Group ambacho kinafuatilia matatizo ya Burundi, kupitia tovuti yao, kimeandika kuwa chanzo cha mgogoro huo ni uchaguzi mkuu wa Julai 2015.

Rais Nkurunziza

Ripoti hiyo imeeleza kuwa katika kuchaguliwa tena Rais Nkurunziza, ambaye unatokana na uamuzi wake wa Aprili wa kugombea tena madaraka, ndio uliosababisha machafuko nchini Burundi.

Pia uamuzi wake umefanya kutokuwepo maendeleo yoyote katika hatua za usuluhishi, na kufanya mgogoro huo kugeuka kuwa ni fukuto la matatizo ya chini kwa chini.

Takriban Waburundi 400,000 wamekimbilia nje ya nchi. Tangu jaribio la kuipindua serikali Mei 2015, siasa za kuwagawanya watu zimesababisha uvunjifu wa amani ndani ya jeshi, imesema ripoti hiyo.

Jeshi limegawanyika

Kwa mujibu wa ripoti kumekuwa na mlolongo wa vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyoelekezwa kwa maafisa kadhaa; wale ambao wako upande wa utashi wa kisiasa wa rais na wenye kushukiwa kuwa wanasikitiko na waliokuwa wamepanga mapinduzi. Harakati za utawala huo kuwaua watu pia zimekuwa zinaendelea ughaibuni.

Ripoti imeongeza kuwa jeshi hilo ambalo limegawanyika na kushuka morali ni tishio kubwa kwa utulivu wa nchi hiyo. "Nikupitia mazungumzo ya kweli, ambayo yanahitajika hivi leo kuliko wakati wowote mwengine, kati ya serikali na upande wa upinzani, unaweza kuwapatia uhakika maafisa ambao wana wasiwasi juu ya kuingizwa siasa katika taasisi ya jeshi," imesema ripoti hiyo.

Historia ya jeshi

Kufuatia misaada ya nje kulisaidia jeshi kufanya mabadiliko kwa zaidi ya miaka 10, sifa ya jeshi hilo imekumbwa na dosari kubwa. Mafunzo ya kimataifa yamemalizika, na ubora wa jeshi hilo katika kushiriki katika shughuli za kulinda amani bado unatiliwa mashaka.

XS
SM
MD
LG