Jeshi la Misri limeidhinisha uhamishaji wa madaraka kutoka kwa Rais Hosni Mubarak hadi kwa Makamu Rais Omar Suleiman na kutoa wito wa kurejeshwa kwa hali ya kawaida katika mji Cairo ambao umekumbwa na maadamano kwa siku ya 18 sasa.
Jeshi lilitoa taarifa Ijumaa baada ya kukutana na Baraza Kuu katika siku ambapo waandaaji wa maandamano wanatabiri maandamano makubwa zaidi tangu kuanza kwa upinzani huo.
Taarifa ya jeshi ilisema jeshi litahakikisha kuwa mageuzi yaliyopendekezwa na Bwana Mubarak yanatakelezwa, ikiwa ni pamoja na kuondoa hali ya tahadhari iliyokuwepo kwa miaka 30 na kuwezesha serikali ya Misri kuwadhibiti kikamilifu wananchi wa Misri.
Alhamisi Mubarak aliwakasirisha waandamanaji alipotoa hotuba bila kusema anajiuzulu. Maelfu kwa maelfu ya watu wamejitokeza Ijumaa kwa maandamano zaidi ikiwa ni ishara wazi kuwa mgogoro wa Misri bado haujamalizika.