Wanajeshi watiifu kwa serikali ya muungano ya Libya GNA, wametoa taarifa inayoeleza kwamba wamechukua udhibiti wa makao makuu ya kundi la Islamic State katika mji wa Sirte.
Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga kwa lengo la kuiondoa Islamic State kutoka Sirte, mji muhimu wa Pwani ambao umekuwa ngome ya operesheni za kundi hilo la kigaidi.
Maafisa wa serikali ya marekani walisisitiza siku ya Jumatano kwamba hakuna wanajeshi wake ambao wanahusika katika mapigano ya moja kwa moja ardhini.