Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 09:25

Jeshi la Zimbabwe kutotambua kiongozi mwingine yeyote isipokuwa Mugabe -Tsvangrai


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe,akisalimiana na wananchi wanaomuunga mkono katika eneo la Mutare, Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe,akisalimiana na wananchi wanaomuunga mkono katika eneo la Mutare, Zimbabwe.

Rais Robert Mugabe asema ataitisha uchaguzi mkuu ikiwa kuna katiba mpya au la wakati huo huo jeshi la nchi hiyo limesema halitaki kutambua kiongozi mwingine yeyote.

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo wamemwambia hawatamruhusu mtu yeyote isipokuwa rais Robert Mugabe kuongoza nchi hiyo, bila kujali nani anashinda uchaguzi.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi katika mji mkuu Harare Bw.Tsvangirai amesema yeye na chama chake cha MDC hawataki vita na ndio maana wanasisitiza mageuzi ya kikatiba kabla ya uchaguzi kufanyika.

Rais Robert Mugabe ameahidi kuitisha uchaguzi mwaka huu, ikiwa kama kuna katiba mpya au hakuna. Lakini Bw. Tsvangirai anasisitiza kwamba Bw.Mugabe hawezi kuitisha uchaguzi peke yake.

Lakini wiki iliyopita Bw.Tsvangirai na Bw.Mugabe waliweka tarehe ya mwisho kuwa Machi 15 kwa ajili ya kamati ya katiba kuwasilisha rasimu ya awali.

XS
SM
MD
LG