Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 21:14

Jeshi la Ukraine linasema limedungua ndege zisizo na rubani 32 za Russia


Vifaru vya jeshi la Ukraine vyaonekana katika mazoezi kwenye kambi ya kijeshi katika mkoa wa Zaporizhzhia, Aprili 5, 2023.

Wizara ya ulinzi wa Ukraine Jumanne ilisema wanajeshi wake walidungua ndege zisizo na rubani 32 kati ya 35 zilizotengenezwa Iran ambazo zilitumiwa na Russia katika shambulio la anga lililolenga Kyiv na miji mingine ya Ukraine.

Jeshi la anga la Ukraine limesema mkoa wa Kyiv ndio uliolengwa zaidi.

Mkuu wa utawala wa kijeshi katika mji wa Kyiv, Serhiy Popko amesema kwenye mtandao wa Telegram kwamba ndege hizo zisizo na rubani zilitokea katika maeneo mengi.

Katika mkoa wa Lviv magharibi mwa Ukraine, gavana Maksym Kozytskiv amesema Russia ilitumia ndege zisizo na rubani kushambulia kituo muhimu cha miundobinu ya mawasiliano.

Maafisa katika mji wa Zaporizhzhia wameripoti pia mashambulizi ya makombora ya Russia kwenye miundombinu ya mawasiliano na maeneo ya kilimo.

Forum

XS
SM
MD
LG