Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 03:16

Jeshi la Ukraine limetungua ndege 24 zisizokuwa na rubani za Russia


Mfano wa Drone za Russia
Mfano wa Drone za Russia

Jeshi la anga la Ukraine limesema uingiliaji kati ulifanyika katika mikoa  ya Dnipropetrovsk, Kharkiv na mingineyo.

Jeshi la Ukraine limesema leo Jumatatu kuwa limetungua ndege zote 24 zisizokuwa na rubani ambazo Russia ilizitumia katika mashambulizi ya usiku kucha zikilenga maeneo mbali mbali nchini humo.

Jeshi la anga la Ukraine limesema uingiliaji kati ulifanyika katika mikoa ya Dnipropetrovsk, Kharkiv, Kirovohrad, Kyiv, Poltava, Sumy na Vinnytsia. Serhiy Lysak, gavana wa Dnipropetrovsk, alisema kwenye mtandao wa Telegram mashambulizi ya Russia yaliwajeruhi watu wawili na kuharibu majengo ya nyumba pamoja na shamba.

Maafisa wa Kharkiv waliripoti uharibifu wa miundombinu ya raia. Katika mkoa wa Belgorod nchini Russia, katika mpaka wa Kharkiv, maafisa wamesema Jumatatu kuwa shambulio la Ukraine ambalo lilimjeruhi mtu mmoja na kuharibu majengo manne ya ghorofa katika mji wa Shebekino.

Forum

XS
SM
MD
LG