Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:01

Jeshi la Ufaransa lamuua kiongozi wa islamic State eneo la Sahara

Askari mmoja wa Jeshi la Ufaransa akifuatilia eneo la mashambani wakati wa operesheni ya Barkhane kaskazini mwa Burkina Faso Novemba 10, 2019.
Askari mmoja wa Jeshi la Ufaransa akifuatilia eneo la mashambani wakati wa operesheni ya Barkhane kaskazini mwa Burkina Faso Novemba 10, 2019.

Jeshi la ufaransa limesema limemuuwa mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya wafaransa sita wafanyakazi wa misaada na walinzi wao raia wa Niger mwaka jana huko Niger.

Jeshi la ufaransa limesema limemuuwa mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya wafaransa sita wafanyakazi wa misaada na walinzi wao raia wa Niger mwaka jana huko Niger.

Katika taarifa iliyotolewa jumanne , wizara ya ulinzi imemtaja mtu aliyeuwawa jumatatu kuwa ni Soumana Boura kiongozi wa kundi la Islamic state katika eneo la Sahara ambaye aliongoza kundi lenye dazeni ya wapiganaji magharibi mwa Niger.

Wanachama hao sita wa shirika lisilo la kiserikali ACTED na walinzi wao waliuwawa mwezi augusti mwaka 2020 walipokuwa wanatembelea mbuga ya taifa ya Wanyama ya Koure , iliyoko kilomita 65 kutoka mji mkuu wa Niger, NIAMEY.

Taarifa ya wizara imesema Boura alipiga picha ya video mauaji ya waathirika hao nane na kusimamia uchapishaji wa picha hizo. Msemaji wa wizara hiyo kanali Pascal Lanni ameiambia AFP Boura aliuwawa na shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani wakati akiendesha pikipiki yake.

XS
SM
MD
LG