Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:06

Jeshi la Sudan lapambana na waasi.


Wapiganaji wa Sudan Kusini.
Wapiganaji wa Sudan Kusini.

Mapambanao makali yazuka katika mji wa al Damazin katikam jimbo la Blue Nile kati ya majeshi yanaounga mkono kusini na yale ya Sudan.

Jeshi la Sudan limepambana na waasi walioungana na jamhuri mpya huru ya Sudan Kusini katika jimbo muhimu la mpakani.

Mapigano hayo yalizuka alhamisi usiku katika mji wa al Damazin katika jimbo la Blue Nile, na kila upande umemlaumu mwenzake kwa kuchochea ghasia.

Serikali ya Sudan ilisema leo imerudisha nyuma shambulizi la wanajeshi wanaounga mkono chama tawala cha Sudan kusini (SPLM).

Tawil la kaskazini la SPLM lilidai kuwa jeshi la Sudan lilishambuilia maeneo ya majeshi yanayounga mkono kusini.

Ghasia za hivi karibuni zimeongeza wasi wasi kuwa mapigano kati ya pande hizo mbili yanasambaa kutoka jimbo la Kordofan Kusini ambalo pia lipo karibu na mpaka.

XS
SM
MD
LG