Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:23

Jeshi la Sudan lakamata ngome ya waasi


Rais wa Sudan Omar al-Bashir (kulia) akiwa na mwenzake wa kusini Salva Kiir .

Jeshi la Sudan limekamta ngome ya waasi katika operesheni zao Kordofan kusini na Abyei.

Jeshi la Sudan linasema limekamata ngome moja ya waasi katika mpaka ulio na ghasia wa jimbo la Blue Nile.

Maafisa wa Sudan walisema jeshi limefanikiwa katika kuwasukuma nyuma waasi nje ya Kurmuk mji ulio karibu na Sudan Kusini ambayo wamejitenga na Sudan mwezi July. Wamesema mji huo umeokolewa wote kutoka kwa majeshi yanayounga mkono jirani zao wa kusini.

Pamoja na Blue Nile , majeshi ya Sudan yalifanya operesheni dhidi ya shughuli za waasi katika majimbo mengine mawili Kordofan kusini na Abyei, majimbo yenye utajiri wa mafuta kwenye mpaka kati ya nchi hizo.

XS
SM
MD
LG