Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:12

Jeshi la Ethiopia lazingira kijiji nchini Sudan Kusini


Kijana wa kabila la Luo Nuer akiwa amebeba bunduko huku akitembea kwenda nyumani kwenye jimbo la Yuai Uror, Sudan Kusini Julai 23, 2013.
Kijana wa kabila la Luo Nuer akiwa amebeba bunduko huku akitembea kwenda nyumani kwenye jimbo la Yuai Uror, Sudan Kusini Julai 23, 2013.

Jeshi la Ethiopia limsema limeingia Sudan Kusini na kuzingira vijiji ambapo zaidi ya watoto 100 waliotekwa Ethiopia wanashikiliwa huko.

Watoto hao walitekwa wakati washukiwa wapiganaji wa Murle waliposhambulia vijiji huko Ethiopia kusini magharibi katika eneo la Gambella Ijumaa. Waziri wa mambo ya nje wa muda, Peter Bashiri Gbandi, amesema jeshi la Sudan Kusini halikuhusika na shambulizi la Ijumaa.

Baba Medan, Gavana wa jimbo la Boma ambapo watu wa Murle wanapoishi, aliwashutumu wapiganaji wa kikundi cha Cobra, kikosi cha wanamgambo wa zamani katika eneo hilo kwa shambulizi hilo.

Uasi wa Cobra dhidi ya serikali ya Sudan Kusini ulianza 2011 hadi 2013.

XS
SM
MD
LG