Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:41

Jeshi la Rwanda lawasimamisha kazi maofisa wake wanne


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Jeshi limesema maofisa watatu na kanali mmoja wanafanyiwa uchunguzi kwa utovu wa nidhamu

Jeshi la Rwanda limewasimamisha kazi maofisa wanne wa vyeo vya juu na kuwaweka katika kifungo cha nyumbani kwa tuhuma za kushiriki katika biashara ya magendo ya madini huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Jeshi limesema maofisa watatu na kanali mmoja wanafanyiwa uchunguzi kwa utovu wa nidhamu. Jeshi limesema maofisa hao wananne wanatuhumiwa kwa kushiriki katika biashara ya magendo ya madini pamoja na raia wa Congo.

Umoja wa Mataifa uliwahi kuishutumu Rwanda kwa kuingiza kimagendo madini kama vile bati kutoka DRC. Lakini Rwanda imekanusha kuhusika na biashara kama hizo.

Serikali ya DRC ina udhibiti mdogo wa migodi ya madini katika majimbo ya mashariki karibu na mpaka wa Rwanda.

Miongoni mwa maofisa waliokamatwa ni mkuu wa kitengo cha ujasusi cha jeshi , Brigedia Jenerali Richard Rutatina, aliyewahi kuwa mshauri wa masuala ya usalama wa rais Paul Kagame.

XS
SM
MD
LG