Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 09:31

Jeshi la polisi lachunguza mlipuko Tanzania


Lucas Makondya
Lucas Makondya

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha mlipuko uliotokea katika ofisi za wanasheria za kampuni ya mawakili ya IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia lJumamosi.

Mkondya amesema polisi wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.

“Tupo hapa eneo la tukio, uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama bomu limehusika,” amesema Mkondya.

Ameeleza hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani.

“Tuwaachie Jeshi la Polisi wafanye kazi yao,” amesema Magai.

Ofisi za wanasheria wa kampuni hiyo zipo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

Kwa upande wao vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema kuwa ofisi za kampuni ya mawakili IMMMA Advocates zimewaka moto Jumapili alfajiri Jijini Dar es Salaam, na mpaka sasa chanzo hakijajulikana.

Baadhi ya watu wanaoishi katika sehemu hiyo karibu na ofisi hizo Dar es Salaam wanasema walisikia misururu ya milipuko mikubwa muda wa saa nane alfajiri na muda mchache baadaye jumba hilo likajaa moshi na vifusi.

Mmoja ya mawakili wa kampuni hiyo amesema kuwa ofisi yao iliharibiwa lakini hakuna kilichoibiwa.

“Tumepata janga kubwa, ofisi yetu imeharibiwa vibaya kutokana na mlipuko huo,” amesema Fatma Karume.

XS
SM
MD
LG