Jeshi la Nigeria limesema limefanya mashambulizi ya anga Alhamis ambayo yalipiga kambi za wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi na kuuwa idadi kubwa ya wanamgambo.
Katika taarifa maafisa wa Nigeria walisema, jeshi la anga la Nigeria limelenga kambi za kijeshi za Boko Haram na kambi ya silaha katika msitu wa Sambisa na mji wa Gwoza ngome kuu mbili za kundi hilo la Boko Haram.
Limesema baada ya mashambulizi hayo wanamgambo wengi walikuwa walianza kutoroka ngome zao.Lakini taarifa hizo hazikuweza kuthibitishwa na wasiofungamana na upande wowote juu ya taarifa hizo za kijeshi.