Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:26

Jeshi la Nigeria laokoa wanafunzi na wafanyakazi huko Kuriga

Jeshi la Nigeria likishika doria karibu na Shule ya Msingi na Sekondari ya LEA Kuriga ambako wanafunzi walitekwa nyara huko Kuriga, Kaduna, Nigeria, Jumamosi, Machi 9, 2024. (Picha ya AP/Jumapili Alamba)

Jeshi la Nigeria Jumapili liliokoa wanafunzi na wafanyakazi ambao walitekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule moja kaskazini mwa nchi hiyo mapema mwezi huu, jeshi lilisema, siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya kulipa fidia ya $ 690,000.

Utekaji nyara wa wanafunzi 287 Machi 7 huko Kuriga katika jimbo la kaskazini-magharibi la Kaduna, ulikuwa wa kwanza katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika tangu 2021 wakati zaidi ya wanafunzi 150 walichukuliwa kutoka shule ya sekondari huko Kaduna.

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Edward Buba alisema mateka 137 wanawake 76 na wanaume 61 waliokolewa alfajiri ya Jumapili katika jimbo jirani la Zamfara.

Chanzo cha usalama kilisema awali wanafunzi hao walikuwa wameachiliwa huru msituni na walikuwa wakisindikizwa hadi mji mkuu wa Kaduna kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kuunganishwa na familia zao.

Forum

XS
SM
MD
LG