Mahakama katika Jimbo la Rakhine mwishoni mwa Juni ilimhukumu miaka mitano gerezani na kazi ngumu Htet Aung, ripota wa shirika la habari la Development Media Group (DMG).
Mlinzi wa shirika la habari, Soe Win Aung, alipewa hukumu kama ya Aung. Wote wawili wameshtakiwa chini ya sheria ya kukabiliana na ugaidi ya Myanmar, na hukumu hiyo haikuwekwa wazi mara moja.
Waangalizi wa kimataifa na DMG wamelaani hukumu hizo. Wakiita hukumu isiyo ya haki, shirika la uangalizi wa vyombo vya habari la Reporters Without Borders, au RSF, limesema serikali ya Myanmar inalenga kwa makusudi wafanyakazi wa DMG, chombo kinachofichua uhalifu wa kijeshi.
Mhariri wa DMG, Nay Win San amelezea hukumu hizo kuwa kali na kusema wanajeshi hawakutoa ushahidi kamili.
Forum