Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 20:05

Jeshi la Myanmar laua watu 50 katika shambulizi la anga-Vyombo vya habari


Picha hii iliyotolewa na kundi la wanaharakati yaonyesha hali ilivyokuwa baada ya shambulizi la anga la jeshi la Myanmar katika mkoa wa Sagaing, Aprili 11, 2023

Takriban watu 50 waliuawa Jumanne katikati mwa Myanmar katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi kwenye hafla iliyohudhuriwa na wapinzani wa utawala wa nchi hiyo, kulingana na vyombo vya habari na wanachama wa vuguvugu la kujihami katika eneo hilo.

Zikinukuu wakazi katika mkoa wa Sagaing, BBC idhaa ya Kiburma, Radio Free Asia (RFA), na gazeti la mtandaoni Irrawaddy, ziliripoti kuwa kati ya watu 50 na 100, wakiwemo raia walifariki katika shambulizi hilo.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha mara moja ripoti hizo na msemaji wa utawala wa kijeshi hakujibu ombi kwa njia ya simu kwa ajili ya kupata maelezo.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres alitoa taarifa akilaani vikali mauaji hayo na kutoa wito wa kuwajibishwa wahusika, msemaji wake amesema, akiongeza kuwa Guterres amerejelea wito wake kwa jeshi kusitisha kampeni ya ukatili dhidi ya wanainchi wa Myanmar nchini kote.

Jeshi lilikanusha tuhuma za kimataifa kwamba lilitekeleza ukatili dhidi ya raia na kusema linapambana na “magaidi” wenye dhamira ya kuyumbisha usalama wa nchi.

XS
SM
MD
LG