Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:54

Jeshi la Marekani lamuua kiongozi wa ISIS nchini Somalia


Wanajeshi wa Marekani waonekana wakiwa na kikosi cha Somalia huko Danab, Mei 9, 2021.
Wanajeshi wa Marekani waonekana wakiwa na kikosi cha Somalia huko Danab, Mei 9, 2021.

Jeshi la Marekani liliendesha operesheni ambayo ilimuua kiongozi wa kundi la Islamic State kaskazini mwa Somalia, maafisa wa Marekani wamesema Alhamisi.

Maafisa hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wamewaambia waandishi wa habari kwamba Bilal al-Sudani, aliyetajwa na Marekani kama kiongozi wa ISIS nchini Somalia, aliuawa katika operesheni pamoja na washirika wake 10.

Wameongeza kuwa operesheni hiyo iliidhinishwa na Rais Joe Biden mapema wiki hii na kuendeshwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Maafisa hao walikataa kutoa maelezo ya msingi kuhusu operesheni hiyo. Walikataa kuelezea tishio lolote la moja kwa moja lililosababishwa na Sudani kwa Marekani, ikiwa taarifa zozote za kijasusi zilikusanywa, jinsi jeshi la Marekani lilivyoendesha operesheni hiyo au ni wanajeshi wangapi walihusika katika operesheni hiyo.

XS
SM
MD
LG