Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 14:33

Jeshi la Israel laushambulia vikali mji wa Rafah huko Gaza


Moto wazuka kufuatia mashambulizi ya anga ya Israek huko Rafah ukanda wa Gaza, Novemba 13,2023. Picha ya AFP
Moto wazuka kufuatia mashambulizi ya anga ya Israek huko Rafah ukanda wa Gaza, Novemba 13,2023. Picha ya AFP

Israel imefanya mashambulizi ya anga katika mji wa Gaza wa Rafah baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuamuru jeshi lake kufanya mpango wa kuwahamisha raia kutoka mji huo wa mpaka wa kusini kabla ya mashambulizi ya ardhini yanayotarajiwa.

Shirika la habari la Associated Press, likinukuu maafisa wa afya na mashahidi, limeripoti kwamba watu 28 waliuawa wakati nyumba kadhaa katika eneo la Rafah ziliposhambuliwa. AP imesema watoto ni miongoni mwa waliouawa.

Ofisi ya Netanyahu Ijumaa ilisema jeshi lilipewa amri ya kuandaa mpango wa kuwahamisha raia huko Rafah na kutokomeza vikosi vinne vya jeshi la Hamas ambavyo vilikuwa huko.

“Haitawezekana kufikia lengo la vita vya kuitokomeza Hamas kwa kuiachia kambi zake nne za kijeshi huko Rafah,” Netanyahu alisema katika taarifa, akiongeza kuwa “kinyume chake, ni wazi kwamba operesheni kali huko Rafah zinahitaji raia kuondoka kwenye maeneo ya mapigano.”

Taarifa hiyo haikueleza lini mpango huo utaanza kutekelezwa na wapi zaidi ya Wapalestina milioni 1.4 watahamishiwa, huku maafisa wa Umoja wa mataifa wakisema mara kadhaa kwamba hakuna sehemu yoyote iliyo salama huko Gaza.

Netanyahu alisema wiki hii kwamba Rafah na mji wa Khan Younis ndizo ngome mbili za mwisho za Hamas.

Forum

XS
SM
MD
LG