Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:17

Jeshi la DRC lathibitisha kuwashilikia wanajeshi wawili wa Rwanda


Jeshi la DRC likifanya doria baada ya kuwafurusha waasi wa M23 huko Kibumba, Picha iliyopigwa na mwandishi wa VOA Austere Malivika
Jeshi la DRC likifanya doria baada ya kuwafurusha waasi wa M23 huko Kibumba, Picha iliyopigwa na mwandishi wa VOA Austere Malivika

Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumapili limethibitisha kwamba linawashikilia wanajeshi wawili wa Rwanda siku moja baada ya Kigali kuishutumu DRC kuunga mkono waasi waliowateka nyara wanajeshi hao.

Jumamosi, Rwanda ilidai kuwa wanajeshi wake wawili walitekwa nyara na waasi wa Kihutu wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC.

Lakini jeshi la DRC lilisema wanajeshi hao walivuka mpaka na kuingia kwenye ardhi ya Congo na wamezuiliwa na wenyeji.

Kila serikali huishutumu nyingine mara kwa mara kuunga mkono makundi ya waasi ambayo inataka kuyatokomeza.

Brigadia Jenerali Sylvain Ekenge amesema kukamatwa kwa wanajeshi hao wawili ni ushahidi kuwa jeshi la Rwanda linaendesha operesheni zake kwenye ardhi ya Congo.

“Kulingana na maelezo ya wanajeshi hao, waliingia kwenye ardhi ya Congo Jumatano tarehe 25 Mei kushambulia kambi ya jeshi la Congo ya Rumangabo, umbali wa zaidi ya kilomita 20 kutoka mpaka wa Rwanda,” Ekenge amesema.

“Baada ya kufurushwa na jeshi la DRC huko Rumangabo, walipotea na hatimaye walikamatwa na wenyeji, amesema Ekenge ambaye ni msemaji wa jeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini, ambako Rumangabo inapatikana.

Jeshi la Rwanda lilitoa wito kwa viongozi mjini Kinshasa kufanya wawezalo ili wanajeshi wake waachiliwe, likisema walitekwa nyara wakati wakifanya doria ya kuwasaka waasi wa Rwanda wa kundi la Kihutu la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda( FDLR) na baadaye wakachukuliwa na kuvushwa mpaka ndani ya DRC.

XS
SM
MD
LG