Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:30

Mwingine aokolewa kutoka kwenye jengo lililoanguka jijini Nairobi


Waokozi wa Msalaba Mwekundu wakimtoa mwanamke kwenye kifusi cha jengo lililoanguka mjini Nairobi hivi karibuni.
Waokozi wa Msalaba Mwekundu wakimtoa mwanamke kwenye kifusi cha jengo lililoanguka mjini Nairobi hivi karibuni.

Wafanyakazi wa uokozi mjini Nairobi, Kenya wameokoa mtu mwingine aliyenusurika katika jengo lililoanguka mtaa wa Huruma karibu wiki moja iliyopoita na kuuwa watu 26.

Pius Masai, ambaye ndiye kiongozi wa operesheni ya uokozi, aliwaambia waandishi wa habari leo kwamba mwanamke waliyempata mpaka sasa bado amebanwa katika vifusi lakini ameweza kuongea na wafanyakazi wa uokozi ambao wamekaa tayari kumsaidia mara tu atakapotolewa.

Masai aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mwanamke huyo hangeweza kusogea lakini alikuwa salama. Siku ya Jumanne waokozi hao waliokoa mtoto mmoja kutoka kwenye vifusi baada ya siku kadhaa za mvua nchini humo.

Shirika la msalaba mwekundu lilimpata baba ya mtoto huyo ambaye alitambuliwa kuwa ni Dealeryn Wasike mwenye umri wa miezi 6. Wasike alilazwa hospitali na waandishi walielezwa alikuwa ameishiwa maji na hakuwa na majeraha makubwa.

XS
SM
MD
LG