Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 11:19

Jengo laporomoka Nairobi, watu 15 hawajulikani waliko


Watu washuhudia jengo la ghorofa saba lililoporomoka kwenye mtaa ulio mjini Nairobi, Kenya mnamo tarehe 13 Mei, 2017. Picha imepigwa na Kennedy Wandera/VOA.

Jengo la ghorofa saba liliporomoka usiku wa kuamkia Jumanne, katika kitongoji kimoja cha mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Mkasa huo ulitokea katika kijiji cha Kware Pipeline, mtaa wa Embakasi, nje ya mji wa Nairobi.

Kufikia jioni ya Jumanne, takriban watu 15 hawakuwa wanajulikana waliko kufuatia mkasa huo.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, lilisema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa makundi ya uokozi yalikuwa kwenye eneo la mkasa.

Mashahidi wameiambia Sauti ya Amerika kwamba magari ya msalaba mwekundu na ambulensi kadhaa zilionekana zikisafirisha watu kutoka eneo la tukio hilo.

Halmashauri ya kupambana na majanga ilisema Jumanne kwamba baadhi ya wakazi walikuwa wametoroka baada ya kuonywa kwamba jengo hilo lilikuwa kwenye hatari ya kuporomoka.

Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, takriban watu 49 walikufa baada ya jengo jingine kuporomoka mjini Nairobi.

Habai zaidi zitafuata.

XS
SM
MD
LG