Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 10:18

Jean-Piere Bemba ahukumiwa miaka 18 jela


Jean-Pierre Bemba Gombo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Majaji wa mahakama ya ICC huko The Hague walitoa hukumu ya miaka 18 jela siku ya Jumanne katika kesi ya kiongozi wa zamani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Jean-Pierre Bemba.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bwana Bemba ambaye wakati fulani alikuwa Makamu Rais wa DRC alifunguliwa mashtaka kwa kufumbia macho ubakaji wa wanajeshi wake katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati anaendesha uasi kati ya Oktoba 2002 na Mei 2003.

Alikutwa na hatia mwezi Machi katika mashitaka matano ya uhalifu wakati wa vita baada ya kupeleka wanajeshi wake Jamhuri ya Afrika ya Kati-CAR kuzima uasi dhidi ya Rais Ange Felix-Patassi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG