Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:21

Jawara, Rais wa kwanza wa Gambia amefariki akiwa na miaka 95


Dawda Kairaba Jawara, Rais wa kwanza wa Gambia
Dawda Kairaba Jawara, Rais wa kwanza wa Gambia

Jawara aliunda chama cha PPP huko Gambia ambacho kiliongoza hadi taifa hilo lilipopata uhuru wake mwaka 1965. Ofisi ya Rais aliyeko madarakani nchini Gambia imemuita Jawara kuwa ni Baba wa taifa la Gambia

Rais wa kwanza baada ya uhuru wa Gambia, Dawda Kairaba Jawara ambaye aliongoza taifa hilo dogo lililopo Afrika magharibi kwa miaka 24 kabla ya kuondolewa kwa mapinduzi mwaka 1994 amefariki akiwa na umri wa miaka 95.

Ofisi ya Rais wa Gambia Adama Barrow aliyechaguliwa katika uchaguzi wa mwaka 2016 na kumaliza utawala wa ofisa wa jeshi ambaye alimuondoa madarakani Jawara, Yahya Jammeh ulimuelezea marehemu rais huyo kama mzee mwenye kuheshimiwa na Baba wa taifa la Gambia.

Jawara daktari wa wanyama aliunda chama cha PPP mwaka 1959 ambacho kiliongoza taifa hilo hadi uhuru wake mwaka 1965. Alikuwa Waziri Mkuu wa nchi kuanzia mwaka 1962 hadi 1970 kabla ya kubadili katiba ya nchi hiyo na kuwa Jamhuri mwaka 1970 na hatimaye kuwa rais wa kwanza wa Gambia.

XS
SM
MD
LG