Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:21

Jeshi la Seoul: Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kuruka


Medics transport a patient through heavy rain into an ambulance at Life Care Center of Kirkland, the long-term care facility linked to several confirmed coronavirus cases in the state, in Kirkland, Washington, March 7, 2020.
Medics transport a patient through heavy rain into an ambulance at Life Care Center of Kirkland, the long-term care facility linked to several confirmed coronavirus cases in the state, in Kirkland, Washington, March 7, 2020.

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Jaribio la Korea Kaskazini kurusha kombora mapema Jumapili kutoka katika Bandari ya jiji la Sinpo “linakadiriwa kuwa halikuwa na mafanikio.”

Wanadhimu wa wakuu wa jeshi la Korea Kusini hawakutoa maelezo zaidi kuhusu jaribio la kombora hilo, na wala hakukuwa na taarifa za wazi ni aina gani ya kombora lilifyatuliwa.

Urushaji wa kombora hilo umekuja muda usiozidi masaa 24 baada ya gwaride kubwa la kijeshi kufanyika katika mji mkuu wa Korea Kaskazini ambayo lilishuhudiwa katika miji mikuu mingi ulimwenguni kama ni njia ya serikali ya Kim Jong Un kuonesha nguvu zake za kijeshi.

Shirika la habari la serikali ya Korea Kusini Yonhap limesema kuwa mkuu wa usalama wa taifa ataitisha mkutano wa Baraza la Usalama la Taifa baadae Jumapili ilikufanya tathmini jinsi hali inavyoendelea katika eneo hilo.

Hakukuwa na tamko la mara moja kutoka Washington, ambayo imejihusisha kwa karibu na kushirikisha nguvu za kidiplomasia za kimataifa ilikumshawishi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kusitisha utashi wake wakutengeneza silaha za nyuklia.

Jaribio lililofeli mara moja

Muda mfupi baada ya kurusha kombora, taarifa kutoka kikosi cha Marekani cha Pacific Command zilieleza kuwa kombora hilo liliripuka hapahapo muda sio mrefu na bado inafanyika tathmini kujua ni kombora la aina gani.

Taarifa hiyo pia imesisitiza nia thabiti ya Washington “kushirikiana na washirika wake,” hasa Korea Kusini na Japan, ilikuhakikisha kunaendelea kuwepo usalama katika eneo hilo la rasi ya Korea.

Makamu wa Rais Mike Pence, ambaye alikuwa njiani kuelekea Korea Kusini jioni Jumamosi alipewa muhtasari wa kufeli kwa jaribio hilo la kombora na amezungumza na Rais Donald Trump kama ilivyoeleza taarifa ya ofisi yake.

XS
SM
MD
LG