Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 18:24

UN kujadili jaribio la balistiki la Korea Kaskazini


Kombora la masafa ya kati na marefu la Korea Kaskazini kabla halijarushwa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) litakutana katika kikao chake cha dharura Jumanne kufuatia jaribio la kombora la hivi karibuni lililofanywa na Korea Kaskazini.

Marekani, Japan na Korea Kusini wameomba mkutano wa dharura baada ya Pyongyang kurusha kombora Jumapili katika anga za juu zaidi zisizo za kawaida.

Anga hizo ndizo zinazopita silaha za balistika ikiwa ni kiashiria kwamba Korea Kaskazini tayari iko katika uwezo mpya wa teknolojia inayoendeshwa na nguvu ya nishati na mafuta yenye uwezo wa kupaisha kombora hilo mpaka kilometa 4,500.

Mapema Jumatatu, Korea Kaskazini imesema ilifanikiwa kufanya jaribio la kombora jipya la masafa ya kati na marefu, lililosimamiwa na kiongozi Kim Jong Un, lililokuwa linalenga kupima uwezo wake wa kubeba “vichwa vikubwa vya silaha za nyuklia.”

Shirika la Habari la Serikali KCNA wamesema kombora hilo lilirushwa katika pembe ya juu ili isisababishe madhara kwa usalama wa nchi za jirani na kuruka kilometa 787, na kufikia mnyanyuko wa kilometa 2,111.

Japan na Korea Kusini kwa haraka zililaani jaribio jipya la Korea Kaskazini na kuliangalia kama ni tishio kwa eneo na ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa.

Jaribio hilo kwa mujibu wa tamko la ikulu ya White House, “inalazimu kuwa ni ilani kwa mataifa yote kutekeleza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG