Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:17

Korea Kaskazini yashindwa kufanikisha jaribio la kombora


Raia wa Korea Kusini akiangalia ripoti za TV zikionyesha habari katika gazeti la Korea Kaskazini la Rodong Sinmun.
Raia wa Korea Kusini akiangalia ripoti za TV zikionyesha habari katika gazeti la Korea Kaskazini la Rodong Sinmun.

Korea Kaskazini huenda imefanya jaribio la kombora la masafa ya kati ambalo lilianguka sekunde chache tu baada ya kupaa, katika kile kinachoonekana kama kushindikana kwa mara ya pili kwa jaribio hilo katika muda wa wiki chache.

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini ameripoti kutofanikiwa kwa urushaji huo leo Alhamisi. Tukio hilo limetokea siku chache tu kabla ya mkutano wa ngazi ya juu unaotarajiwa kufanyika Pyongyang wiki ijayo. Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema Korea Kaskazini inafanya jaribio la kombora lake la masafa ya kati, linalojulikana kama MUSUDAN, ambalo linaweza kutumiwa kufikia kambi za kijeshi barani Asia na kwenye bahari ya Pacific.

Jaribio hilo linakuja wakati Korea ya Kusini na Marekani zinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi, ambyo hufanyika ya kila waka, jambo ambalo Korea ya Kaskazini imelitaja kuwa la uchokozi.

XS
SM
MD
LG