Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 15:35

Wanajeshi wa Japan wawasili Sudan Kusini


Japanese peacekeepers arrive at the Juba airport to participate in the United Nations Mission in South Sudan (UNMISS) in South Sudan's capital Juba, Nov. 21, 2016.
Japanese peacekeepers arrive at the Juba airport to participate in the United Nations Mission in South Sudan (UNMISS) in South Sudan's capital Juba, Nov. 21, 2016.

Kikosi cha wanajeshi kutoka Japan kiliwasili nchini Sudan Kusini siku ya Jumatatu, kujiunga na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani, ambacho kimeongezewa majukumu ambayo baadhi ya wakosoaji wanasema huenda yakaifanya Japan kuhuisika katika vita vya nje ya nchi, kwa mara ya kwanza tangu vita vya pili vya dunia.

Wanajeshi hao wapya watasaidia ujenzi wa miundo mbinu kwenye nchi hiyo ambayo haina bandari, na ambayo imeathiriwa mno na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu ilipopata uhuru kutoka kwa nchi ya Sudan.

Lakini kulingana na mamlaka waliyopewa na serikali ya Japan, wanajeshi hao 350 wanaruhusiwa kuwasaidia wafanykazi wa Umoja wa Mataifa na wale wa mashirika ya kutoa misaada, iwapo watakuwa katika hali ya dharura. Aidha kuna mipango ya kuwaruhusu wanajeshi hao, kulinda kambi za Umoja wa Mataifa, ambazo zieshambuliwa wakati wa vita.

XS
SM
MD
LG