Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na mazingira magumu ya kimataifa yanayosababishwa na janga la corona na vita nchini Ukraine, wizara ya mambo ya nje ya Japani imeeleza.
Baadhi ya wakuu wa nchi na serikali 30 wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo katika mji mkuu Tunis, wakati ambapo taifa hilo la Afrika Kaskazini linategemea uagizaji wa bidhaa kutoka huku likiwa linakabiliuwa na hali mbaya ya uchumi.
Mkutano wa nane wa Tokyo wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Afrika (TICAD8) pia unakuja wakati Beijing inaimarisha ushawishi wake katika bara la Afrika na mpango wake wa miundombinu ujulikanaoa kama Belt and Road.
Ni kongamano la kwanza TICAD ambalo hufanyika kila baada ya miaka mitatu ama nchini Japani au nchi ya Afrika tangu janga hili lianze.