Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:17

Japan yatarajiwa kutoa ahadi ya dola bilioni 30 kwa Afrika

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akitoa hotuba katika makazi yake rasmi mjini Tokyo.Xinhua/Zhang Xiaoyu/ REUTERS
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akitoa hotuba katika makazi yake rasmi mjini Tokyo.Xinhua/Zhang Xiaoyu/ REUTERS

Japan inatarajiwa kutoa ahadi ya takriban dola bilioni 30 za misaada kwa ajili ya maendeleo ya Afrika katika mkutano utakaofanyika Tunisia mwishoni mwa wiki, gazeti la Sankei Shimbun litolewalo kila siku limeripoti Ijumaa.

Msaada, ambao utahusu zaidi kuhuse maendeleo ya rasilimali watu ili kuhamasisha ukuaji wa uchumi, utatangazwa kwenye mkutano wa kimataifa wa Tokyo kwa Maendeleo ya Afrika (TICAD) na Waziri Mkuu Fumio Kishida, ambaye atashiriki katika mkutano kwa njia ya mtandao kwa vile bado anapata nafuu kutokana na Covid 19, gazeti hilo limesema.

Serikali haijapatiknaa kutoa maoni kuhusu ripoti hii.

Masuala mengine ni pamoja na usalama wa chakula kwa waafrika kufuatia uvamizi wa Russia nchini Ukraine pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhamasisha biashara rafiki, afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Japan alisema Jumatano.

Mkutano wa nane wa TICAD is wa kwanza tangu mwaka 2019 na ni wa pili pekee kufanyika Afrika. Mkutano huo unaendeshwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia na Tume ya Umoja wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje Yoshimasa atahudhuria mkutano huo na anapanga kukutana na mwenzake wa Tunisia ya Ijumaa kabla ya mkutano mkuu.

XS
SM
MD
LG