Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:10

Japan yaifunga Cameroon 1-0


Keisuke Honda wa Japan akipachika bao la kwanza na la ushindi dhidi ya Cameroon huku golikipa wa Cameroon Souleymanou Hamidou na mabeki wake wakijaribu kumzuia bila mafanikio katika uwanja wa Free State huko Bloemfontein, Afrika Kusini .(Picha na Michae

Wawakilishi wengine wa Afrika katika fainali za kombe la dunia Cameroon –wamepoteza mechi yao ya kwanza baada ya kufungwa 1-0 na Japan.

Wawakilishi wengine wa Afrika katika fainali za kombe la dunia – Cameroon – wamepoteza mechi yao ya kwanza baada ya kufungwa 1-0 na Japan.

Huu ni ushindi wa kwanza wa Japan katika kombe la dunia wakiwa kwenye ardhi ya ugenini baada ya mshambuliaji wake Keisuke Honda kufunga bao la ushindi dhidi ya Cameroon katika kipindi cha kwanza kunako dakika ya 39.

Cameroon ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya ushindi katika mpambano huo lakini walishindwa kutamba kabisa hasa katika kipindi cha kwanza.

Cameroon walionekana kuchanganyikiwa huku mshambuliaji wao hatari Samuel Eto’o akiwa amebanwa vilivyo na wajapan.

Japan hivi sasa ina pointi sawa na Uholanzi wakiongoza kundi E.

Timu nyingine za Afrika ambazo zimepoteza mechi zao za kwanza ni Nigeria na Algeria. Ghana ilishinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Serbia, na wenyeji Afrika Kusini walitoka sare na Mexico

XS
SM
MD
LG