Zaidi ya watu 300 wamejeruhiwa, na watu 15 wameorodheshwa rasmi kama wamepotea.
“Zaidi ya saa 40 zimepita. Hizi ni mbio za kukabiliana na muda na ninahisi kwamba tuko katika wakati muhimu,” Waziri Mkuu Fumio Kishida aliwaambia waandishi wa habari.
Ameongeza kusema kwamba wamepokea ripoti kwamba watu wengi bado wanasubiri kuokolewa chini ya majengo yaliyoporomoka.
Uharibifu kwa kiasi kikubwa uliotokana na tetemeko la ardhi la Jumatatu la kwaingocha 7.6 kwa kipimo cha rikta lililotokea katika mkoa wa Ishikawa, kwenye kisiwa cha Honshu, huku nyumba na majengo mengi yakiharibiwa au kubomoka kabisa na idadi isiyojulikana ya watu wamekwama kwenye vifusi.
Forum