Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 01:51

Japan yaadhimisha miaka 77 tangu tukio la Hiroshima na Nagasaki


Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida wakati wa maadhimisho hayo
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida wakati wa maadhimisho hayo

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida Jumatatu amesisitiza ahadi yake  ya kutoingia vitani wakati wa  katika  hafla iliyojawa na huzuni , ya kuadhimisha  miaka 77 tangu kushindwa kwenye vita vya pili vya dunia.

Katika hotuba yake ya kwanza tangu kuchukua wadhifa wa waziri mkuu mwezi Oktoba , Kishida amesema kwamba Japan itaendelea kushikilia ahadi yake ya kutorudia makosa ya kuingia vitani. Hata hivyo kiongozi huyo hakuzungumzia uchokozi wa Japan katika nusu ya kwanza ya karne ya 20 barani Asia, au waathirika wake.

Suala alilolizungumzia zaidi ni namna Japan ilivyoathirika kwa upande wake baada ya Marekani kuangusha mabomu ya atomic kwenye miji ya Hiroshima na Nagasaki, pamoja na mashambulizi mengine ya mabomu kote nchini ,ukiwemo uwanja wa vita wa Okinawa.

Kishida anaonekana kufuata nyayo za mtangulizi wake aliyeuwawa hivi karibuni Shinzo Abe, ambaye kwa kawaida alikwepa kuzungumzia maovu ya kivita yaliyotekelezwa na Japan wakati wa vita vya dunia. Ingawa Kishida hakufika kwenye eneo la tukio, waziri wake wa usalama wa uchumi Sanae Takaichi na mwenzake wa masuala ya mikasa Kenya Akiba walihudhuria.

XS
SM
MD
LG