Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:30

Japan kukaribisha tena watalii baada ya Covid-19


Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida wakati akiwa mjini London hivi karibuni
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida wakati akiwa mjini London hivi karibuni

Japan imesema Jumanne kwamba itaanza kukaribisha tena makundi ya watalii kama njia ya kurejesha hali ya kawaida baada ya kipindi kirefu cha janga la corona.

Idara ya utalii ya taifa hilo imesema kwamba makundi madogo ya watalii kutoka Australia, Singapore, Thailand na Marekani yatakubaliwa kuingia nchini humo baadaye mwezi huu.

Idara hiyo imeongeza kusema kwamba ziara hizo zitafuata ratiba na kuongozwa kila wakati na watalamu, huku watalii wakihitajika kuwa wamepatiwa chanjo kamili ya covid ikiwemo ile ya booster.

Watalii wa kigeni walizuiliwa Japan tangu mwanzoni mwa janga la corona mwaka 2020. Waziri mkuu Fumio Kishida kwenye hatuba yake mapema mwezi huu mjini London alisema kwamba atarekebisha kanuni za mipaka kuendana na mataifa mengine tajiri kufikia mwezi Juni,bila kutoa maelezo zaidi.

XS
SM
MD
LG