Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:21

Japan: China imekuwa ikifanya ujasusi dhidi yetu kwa kutumia 'puto'


Puto la China lililoangushwa Marekani
Puto la China lililoangushwa Marekani

Wizara ya ulinzi ya Japan imesema kwamba iligundua vitu vitatu vilivyokuwa vikipaa katika anga yake tangu mwaka 2019, moja ya vitu hivyo vilipaa sehemu za kusini magharibi na viwili katika sehemu za kaskazini, na kwamba vinaaminika kuwa 'puto' au baloon za ujasusi za China.

Wizara hiyo imesema kwamba serikali ya Japan iliwasilisha malalamiko kwa serikali ya China ikitaka maelezo ya kina.

Video iliyopeperushwa na televisheni ya taifa ya Japan NTV, imeonyesha kitu kinachoonekana kama balloon, kikiwa katika anga ya Japan.

Video hiyo ilichukuliwa mwaka 2020.

Wabunge kutoka chama tawala cha Japan wamesema kwamba wanafikiria kufanyia marekebisho sheria ya ulinzi ya Japan, inayozuia matumizi ya silaha pasipo swala la dharura au kwa ajili ya kujilinda, na kutoa ruhusa ya silaha kutumika iwapo anga ya Japan inaingiliwa.

XS
SM
MD
LG