Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 02:28

Jaynet Kabila atowa msaada kwa waathiriwa wa vita na ubakaji DRC


Janet Kabila, rais wa wakfu ya Mzee Laurent Kabila, dadake rais Joseph Kabila
Janet Kabila, rais wa wakfu ya Mzee Laurent Kabila, dadake rais Joseph Kabila

Jaynet Kabila amekamilisha ziara ya majimbo matatu ya mashariki ya DRC kutoa msaada kwa wanawake waathiriwa wa ubakaji katika majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Kusini pamoja na jimbo la Oriental.

Miaka miwili baada ya kukusanya msaada kutoka majimbo yote ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jaynet Kabila dada pacha wa rais Joseph kabila, amewasilisha msaada huo kwa familia na waathiriwa wa ubakaji na vita katika majimbo hayo ya mashariki ya Kongo.

Katika mahojiano nadra aliyofanya na mwandishi wetu wa Kinshasa Saleh Mwanamilongo katika mji wa Wacha jimboni Oriental, Bi. Kabila anazungumzia masuala ya maendeleo na changamoto zinazoikabili DRC.

Bi Kabila ni kiongozi wa wakfu ya Mzee Laurent Kabila, inayotowa misaada kwa watu wanaoishi na HIV na Ukimwi na vile vile ni rais wa chama cha wanawake wa eneo la Maziwa Makuu kwaajili ya kudumisha amani.

XS
SM
MD
LG