China inatambua Taiwan kuwa ni sehemu yake chini ya sera ya China moja, na mwezi uliopita ilizindua mazoezi ya kijeshi kuzunguka kisiwa hicho kinachojitawala.
Jamhuri ya Czech, Umoja wa Ulaya na mwanachama wa NATO, inaafiki sera ya China moja, kama EU, lakini maafisa wake wanaendeleza uhusiano wa karibu na Taiwan.
“Kituo cha Czech, nchini Taiwan kitazindua shughuli zake Ijumaa, Juni 14, kwa maonyesho ya picha za Kczech, wizara ya mambo ya nje imeeleza.
Shirika la habari la CTK limemnukuu mkuu wa kituo cha Czech, Jitka Panek Jurkova, akisema raia wa Czech, wanataka kuonekana na kusikilizwa Taipei.”
Wizara ya mambo ya nje ya Czech, ina vituo 28 vinavyotangaza taifa hilo katika nchi 25 ulimwenguni isipokuwa China.
Forum