Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:00

Jamii ya watu wafupi na mashirika yasio ya kiserikali yashinikiza serikali kuwatambua

Taib Abdul Rahman kulia Mkurugenzi wa REACHOUT akiwa na mmoja wa jamii ya watu wafupi huko Mombasa Kenya.
Taib Abdul Rahman kulia Mkurugenzi wa REACHOUT akiwa na mmoja wa jamii ya watu wafupi huko Mombasa Kenya.

Ulimwengu ukiadhimisha siku ya watu wenye vimo vifupi, jamii ya watu hao pamoja na mashirika yasio ya kiserikali yanashinikiza serikali kuwatambua na kuwajumuisha katika nafasi za watu wanaoishi na ulemavu, kama njia ya kukabiliana na unyanyapaa miongoni mwao.

Watu wa vimo vifupi bado wanapitia unyanyapaa na kutengwa katika jamii.

Kenya ina zaidi ya watu 3000 wenye vimo vifupi, huku madaktari wakielezea hofu kuwa watoto milioni 1.2 waliodumaa huenda wakabaki na vimo vifupi ukubwani.

Hii ni kulingana ripoti ya Shirika la Takwimu nchini Kenya,mwaka 2019.

Licha ya siku hii kuadhimishwa kila mwaka , bado jamii ya watu wenye vimo vifupi, wanatengwa na kubaguliwa wanapotafuta ajira na hata katika familia.

Kalimbo Mkala, afisa wa muungano wa watu wenye vimo vifupi Kenya, hakusazwa, yeye alipitia unyanyapaa akiwa mdogo na hata alipokua akitafuta ajira.

Akiwa na taaluma ya uhasibu na balozi wa maswala ya watu wenye vimo vifupi, ameitaka serikali kuwahusisha.

Wakitumia kandanda kuwaleta pamoja na kuhamasisha jamii kuhusu watu wenye vimo vifupi , wanaharakati wa asasi za kijamii wamehimiza haja ya serikali kuwatambua na kuhakikisha wanapewa nafasi sawa katika jamii.

Kwa upande wake Hellen Kaberia, mmoja ya watu wenye vifupi, anaelezea kuwa jamii hiyo iko katika kila taaluma, na amewataka wazazi kutoficha watoto wao wenye vimo vifupi.

Imeandaliwa na Amina chombo VOA Mombasa.

XS
SM
MD
LG