Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:58

Jamhuri ya Congo yachagua rais


Maafisa wa jeshi wakiwa katikia mstari kupiga kura
Maafisa wa jeshi wakiwa katikia mstari kupiga kura

Siku moja kabla ya upigaji kura, Serikali iliamuru makampuni ya simu kufunga huduma zao wakati zoezi la uchaguzi likiendelea.

Wapiga kura katika Jamhuri ya Congo wamechagua rais wa nchi yao Jumapili .

Siku moja kabla ya upigaji kura, Serikali iliamuru makampuni ya simu kufunga huduma zao wakati zoezi la uchaguzi likiendelea.

Waziri wa mambo ya ndani wa jamhuri ya Congo Raymond Zephirin Mboulou alituma barua katika makampuni makubwa mawili ya simu nchini humo akisema kuwa sababu kubwa ya uamuzi huo ni kwa ajili ya usalama wa taifa ambapo inawalazimu kufunga huduma zote za simu ikiwemo ujumbe wa SMS katika siku za Jumapili na Jumatatu.

Nakala ya barua hiyo ambayo imetolewa mitandaoni pia ilieleza idadi kadhaa ya namba ambazo zitaendelea kupata mawasiliano ya simu wakati wa upigaji kura.

Amri hiyo inaweza kuzusha mvutano nchini humo ambako rais wa muda mrefu Denis Sassou Nguesso anagombea tena dhidi ya wapinzani wengine nane akiwemo generali Jean Marie Mokolo.

XS
SM
MD
LG