Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 09:36

Afisa mkuu wa ujasusi Marekani James Clapper ajiuzulu


Afisa mkuu wa ujasusi Marekani James Clappe. Alitangaza nia yake ya kujiuzulu siku ya Alhamisi
Afisa mkuu wa ujasusi Marekani James Clappe. Alitangaza nia yake ya kujiuzulu siku ya Alhamisi

Afisa wa juu wa idara ya ujasusi ya Marekani alisema siku ya Alhamisi kwamba hatoendelea na kazi na rais mteule Donald Trump, na akawaeleza wabunge kwamba tayari ameshawasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Mkurugenzi wa idara ya ujasusi, James Clapper, aliwashangaza watu kwa uamuzi wake huo wa kuondoka katika nafasi yake katika mkutano wa kamati ya bunge ya masuala ya ujasusi.

Alisema kwamba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu juzi usiku, na kuwaambia wabunge kuwa ni kitu ambacho kimemfanya ajisikie vizuri.

Tangazo hilo haraka lilizua fununu kwamba Clapper pengine alikuwa akijaribu kutuma ujumbe kwa utawala ujao wa Trump, lakini msemaji wake alizungumzia kutokuwepo kwa nia hiyo.

XS
SM
MD
LG