Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 07:31

Jaji wa serikali kuu anayesimamia kesi ya Trump aamuru mawakili wake kufika mahakamani Ijumaa

 Rais wa zamani Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni huko Windham, New Hampshire, Marekani, Agosti 8, 2023. REUTERS/Reba Saldan
Rais wa zamani Marekani na mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni huko Windham, New Hampshire, Marekani, Agosti 8, 2023. REUTERS/Reba Saldan

Waendesha mashitaka walisema wanapatikana wiki nzima, huku mawakili wa Trump wakiomba kuahirishwa hadi mapema wiki ijayo.

Jaji wa serikali kuu anayesimamia kesi ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kuhusu mashtaka ya kujaribu kubatilisha uchaguzi wa mwaka 2020 ameamuru mawakili wake na waendesha mashtaka wa serikali kuu kufika mahakamani siku ya Ijumaa kwa ajili ya kusikilizwa ili kusaidia kubainisha jinsi ushahidi unaweza kutumika na kushirikishwa katika kesi hiyo.

Jaji wa Mahakama ya wilaya Tanya Chutkan alipanga kusikilizwa kwa kesi hiyo Ijumaa saa 4 asubuhi saa za Washington muda mfupi baada ya mawakili wa Trump na wajumbe wa ofisi ya Wakili Maalum wa Marekani Jack Smith kutofautia na juu ya wakati wa kupanga shauri hilo.

Waendesha mashitaka walisema wanapatikana wiki nzima, huku mawakili wa Trump wakiomba kuahirishwa hadi mapema wiki ijayo.

Forum

XS
SM
MD
LG