Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 19:09

Jaji wa Mahakama ya rufaa ya New York apinga ombi la Trump la kuahirisha kesi ya jinai dhidi yake


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Jaji mmoja wa mahakama ya rufaa ya New York amepinga ombi la Rais wa zamani Donald Trump, la kuchelewesha kesi yake ya jinai ya Aprili 15, wakati akipambana kuondoa kesi hiyo kutoka mji wa Manhattan, huko New York.

Uamuzi huo ulitolewa Jumatatu, wiki moja kabla ya uteuzi wa jopo la mahakama kuanza. Mawakili wa Trump walikuwa wamewasilisha hoja katika kikao cha dharura, wakidai kwamba kesi hiyo ya kihistoria inapaswa kuahirishwa, wakati wakitetea haja ya kuihamisha kutoka mji wa Manhattan wenye wafuasi wengi wa chama cha Democratic.

Trump amependekeza kupitia jumbe za mitandao ya kijamii kwamba kesi hiyo ihamishiwe Staten Island, jimbo pekee la New York ambalo alishinda katika uchaguzi wa mwaka 2016 na ule wa 2020.

Forum

XS
SM
MD
LG