Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 13:15

Jacob Zuma ahukumiwa kifungo cha miezi 15 jela huko Afrika kusini


Rais wa zamani wa Afrika kusini, Jacob Zuma
Rais wa zamani wa Afrika kusini, Jacob Zuma

Mahakama ya katiba nchini humo haiwezi kufanya chochote isipokuwa kuhitimisha kuwa Zuma ana hatia ya uhalifu wa kudharau mahakama, Jaji Sisi Khampepe alisema. Zuma mwenye miaka 79 anashutumiwa kwa matumizi mabaya ya hazina ya serikali wakati wa utawala wake wa takribani miaka tisa

Mahakama ya juu nchini Afrika kusini, Jumanne ilimpa Rais wa zamani nchini humo Jacob Zuma, kifungo cha miezi 15 jela kwa kudharau mahakama kufuatia kukataa kwake kufika mbele ya wachunguzi wanaoshughulikia shutuma za rushwa.

Mahakama ya katiba nchini Afrika kusini haiwezi kufanya chochote isipokuwa kuhitimisha kuwa Zuma ana hatia ya uhalifu wa kudharau mahakama, Jaji Sisi Khampepe alisema. Zuma mwenye miaka 79 anashutumiwa kwa matumizi mabaya ya hazina ya serikali wakati wa utawala wake wa takribani miaka tisa.

Mizani ya sheria
Mizani ya sheria

Aina hii ya kutokujali na kukashifu ni kinyume cha sheria na lazima adhabu itolewe, Khampepe alisema. Nimeachwa bila chaguo jingine, isipokuwa kumhukumu bwana Zuma kifungo, na ni matumaini kwamba kufanya hivyo kunapeleka ujumbe bila shaka, utawala wa sheria na usimamizi wa haki unashinda.

Tume ya uchunguzi inaongozwa na naibu jaji mkuu, Raymond Zondo. Jopo hilo liliundwa na Zuma mwenyewe kutokana na shinikizo juu ya kashfa zinazoongezeka muda mfupi kabla ya kuondolewa mamlakani mnamo mwaka 2018 na chama tawala cha African National Congress (ANC).

Zuma alitoa ushahidi mara moja pekee hapo Julai mwaka 2019 kabla ya kuacha kuhudhuria mahakamani na baadae kumshutumu Zondo katika tume hiyo kuwa anaupendeleo. Kisha alipuuza mialiko kadhaa ya kufika mahakamani akitoa sababu za matibabu na maandalizi kwa kesi nyingine ya ufisadi.

XS
SM
MD
LG