Rais wa Cote de Voire, Allasane Ouattara ameshinda muhula wa pili na hivyo kubaki madarakani. Ouattara alipata asli mia 83 ya kura kutoka katika uchaguzi wa Jumapili, kwa mujib wa matokeo rasmi yalotangzwa usiku wa kuamkia jana. Ushindi wake hata hivyo, haushangazi, kwani raia wa Cote De Voire wanafurahia hali ya utulivu iliyotandaa nchini humo.
Magari yalipiga honi zao, huku watu wakiwa kwenye pirika za kuelekea kazini, wachhuzi wanauza kahawa kando ya barabara, mitaa ya Abidjan inaonekana kama inavyokuwa siku nyengine yeyote, masaa tu baada ya matokeo kutangazwa.
Hali hiyo ni furaha tosha kwa Tonian Amalam, mkazi wa Abidjan.
Amalam anasema, haijaalishi nani kashinda uchaguzi. Mimi nafurahi tu kuwa tunaweza kutembea barabarani na kuona kuwa hamna ghasia.
Rais Ouattara alimshinda kwa kiwango kikubwa, mpinzani wake mkuu mgombea alopata nafasi ya pili, Pascal Affi N’Guessan, aliyejipatia karibu asli mia 9 tu za kura.
Hapo mwaka 2010 na 2011, Zaidi ya watu elfu 3 waliuwawa kufwatia ghasia za baada ya uchaguzi, pale rais alokuwa madarakani Laurent Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi. Jumuiya ya kimataifa ilikubali matokeo yalooonyesha kuwa Ouattara alikuwa mshindi wa uchaguzi wa November mwaka 2010.
Bw. Gbagbo, kwa sasa yuko huko the Hague, akisubiria kesi dhidi yake juu ya makossa ya uhalifu dhidi ya binadam.