Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 22:33

Ivory Coast yaiomba Mali kuwaachia huru wanajeshi wake 49


Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Kanali Assimi Goita, picha ya AP.
Kiongozi wa kijeshi wa Mali, Kanali Assimi Goita, picha ya AP.

Ivory Coast Jumanne imeiomba Mali kuwaachia huru wanajeshi wake 49, waliokamatwa kinyume cha sheria kwenye uwanja wa ndege wa Bamako na kushtumiwa na maafisa wa Mali kuwa ni mamluki.

Hakuna hata mmoja kati ya wanajeshi hao waliokamatwa ambaye alikuwa na silaha za kivita, imesema taarifa kutoka ofisi ya rais wa Ivory Coast baada ya mkutano wa dharura wa Baraza la usalama wa taifa.

Mali Jumatatu ilisema wanajeshi hao wa Ivory Coast walikuwa na silaha na ni mamluki, ilipowakamata wakiwasili nchini humo.

Viongozi wa Ivory Coast wamesisitiza kwamba wanajeshi hao waliwasili nchini Mali kujiunga na tume ya umoja wa mataifa ya kulinda usalama , MINUSMA.

“Hawa sio wanajeshi wa kulinda usalama wa Umoja wa mataifa, kwa hiyo hawashiriki rasmi kwenye tume ya MINUSMA,” msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Farhan Haq amesema Jumanne.

Lakini walikuwa miongoni mwa vitengo vya usalama wa taifa vilivyotumwa na nchi zinazochangia kusaidia vikosi vyao, ameongeza. “Huu ni utaratibu wa kawaida wa tume za kulinda usalama.”

Serikali ya Mali ilisema wizara yake ya mambo ya nje haikupewa taarifa kupitia njia rasmi, ikilaani ukiuakaji wa wazi wa sheria ya makosa ya jinai inayohusu usalama wa mipaka ya nchi.

XS
SM
MD
LG