Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 21:03

Serikali ya Ivory Coast yawanyang'anya silaha wapiganaji


Serikali ya Ivory Coast inawanyang'anya silaha wapiganaji nchini humo katika juhudi za kuboresha usalama
Serikali ya Ivory Coast inawanyang'anya silaha wapiganaji nchini humo katika juhudi za kuboresha usalama

Afisa mmoja nchini Ivory Coast anasema serikali ya nchi hiyo inawanyang'anya silaha wapiganaji katika juhudi za kuboresha usalama nchini humo

Afisa mmoja wa ulinzi nchini Ivory Coast anasema serikali inawanyang’anya silaha na kuwahamasisha kiasi cha wapiganaji 10,000 katika juhudi za kuboresha usalama.

Chombo cha habari cha serikali Jumatano kilimkariri naibu waziri wa ulinzi Paul Koffi Koffi, akisema utaratibu huo unatakiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka. Waziri huyo ambaye alizungumza Jumanne alisema wapiganaji watakaohusika na utaratibu wataingizwa katika jamii.

Watu kote nchini Ivory Coast walishika silaha wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi katika taifa hilo la Afrika magharibi mapema mwaka huu. Ghasia zilianza baada ya Rais wa wakati huo Laurent Gbagbo aliposhindwa uchaguzi wa mwezi Novemba na Alassane Ouattara, lakini alikataa kuachia madaraka.

Majeshi yanayomuunga mkono Ouattara yalimpindua bwana Gbagbo mwezi April. Serikali ya Ouattara hivi sasa inafanya kazi kuyaunganisha majeshi yake na kuirejesha nchi katika hali ya kawaida.

XS
SM
MD
LG